Babu Tale ni meneja mkubwa inchini tanzania akiwa yuko miongoni mwa mameneja ambao wanasimamia wasanii wa WCB Wasafi.
Na hivi juzi aliweza kumpoteza mke wake ambaye anajulikana kwa jina Shamima ila wengi wanamtambua kwa jina Shammy.Tale na mke wake walibahatika kupata watoto 5, wanne wavulana na msichana mmoja.
Na siku ya mazishi ya mke wa Tale kuna matukio mengi ambayo yaliweza kutokea pale,na kati ya matukio hayo ikiwa ni lile la meneja mwengine wa WCB, Salam SK aliweza kupotezea salamu za mkono kutoka kwa Harmonize.Ila watu wengi wanasema Salam sk hajaonyesha utu kwa hivyo anatakiwa amuombe msamaha Harmonize.
Ila la ajabu ni kuwa Babu Tale baada ya kumzika mke wake siku hiyo hiyo alirudi zake Dar-es-salaam na kuwaacha watu wengi wanajiuliza maswali kwa uamuzi huo na wanadai huenda alimtoa mke wake kafara ili aweze kushinda uchaguzi wa mwaka huu kwa sababu anagombea kiti cha ubunge na huenda alitakiwa afike mjini kwa ajili ya kumalizia tambiko.
Comments