style="display:block"
data-ad-format="fluid"
data-ad-layout-key="-f5+5t+4z-d1+5q"
data-ad-client="ca-pub-6938907706761035"
data-ad-slot="2461853092">
(adsbygoogle = window.adsbygoogle || []).push({});
Siku ya Jumapili, drama ilishuhudiwa katika uzinduzi wa albamu ya mwimbaji Size 8 baada ya Ringtone Apoko kufukuzwa kutoka kwa hafla hiyo na DJ Mo.
Akizungumza na wanahabari, DJ Mo alisema kwamba alichukizwa na hisia za Apoko kwa mkewe na ndiyo sababu alichagua kumfukuza.
"Ikiwa sisi ni marafiki tuwe marafiki. Na ukifeel nikama unaenda kuongea against my wife then unanitouch place wrong. Ikiwa sisi ni marafiki na sisi ni wanaume, tunapaswa kuhakikisha kwamba tunalinda watu wetu. Kwa hivyo Ringtone anajitokeza hapa na kuanza kumshutumu Size 8 kwa mambo ambayo hajafanya, hiyo ni makosa,” DJ Mo alisimulia.
DJ Mo aliongeza kuwa Ringtone anapaswa kuacha kufukuzia kila tukio analoalikwa ama sivyo atakuwa kwenye matatizo makubwa.
“Ni venye tu nimeokoka bure ingekuwa mbaya. Na Ringtone anajua napenda kuweka mipaka yangu. Tena huwezi kuwa mwangalifu katika kila tukio, kwa hivyo unafaa kuanglia, si kila tukio ni yaku-clout chase. Haiwezi kuwa event inaendelea alafu unaita media nje kuwambia ujinga. Ndio maana nililazimika kufanya nilichofanya. Isipokuwa ni watu wangu walinistopisha it could have been bad. Heshimu hustle zangu na naheshimu hustle zako,” alisema DJ Mo.
style="display:block"
data-ad-format="fluid"
data-ad-layout-key="-f5+5t+4z-d1+5q"
data-ad-client="ca-pub-6938907706761035"
data-ad-slot="2461853092">
(adsbygoogle = window.adsbygoogle || []).push({});
DJ Mo alikabiliana na Ringtone wakati alipokuwa akimshutumu Size 8 kwa kumnyima nafasi ya kuzungumza kwenye mimbari.
"Ninatoka kwenye uzinduzi huu wa Albamu kwa sababu tumekuja hapa kusaidia Size 8, lakini yeye anawaita watu wa Mungu kwenda kwenye mimbari na kuweka wakfu albamu yake. Wachungaji walipoenda kwenye mimbari nilijiunga nao kwa sababu mimi pia nina mimbari yangu mwenyewe, mimi ni mhudumu. Wachungaji hawana cheo cha juu zaidi kuliko mwanamuziki kama mimi.
“Lakini nilipanda jukwaani kisha Size 8 akanifukuza akisema hiki ni kikao cha mchungaji pekee, nataka niseme size 8, mimi pia ni mpakwa mafuta wa Mungu nimeokoka hadi sasa, nimekata tamaa sana kwa sababu. Size 8 alinifukuza kutoka kwenye mimbari,” alilalamika Ringtone kabla ya DJ Mo kumkabili.
style="display:block"
data-ad-format="fluid"
data-ad-layout-key="-f5+5t+4z-d1+5q"
data-ad-client="ca-pub-6938907706761035"
data-ad-slot="2461853092">
(adsbygoogle = window.adsbygoogle || []).push({});
Ringtone aliendelea kudai kuwa angetuza Size 8 na Sh200,000 lakini akafukuzwa kabla ya kutoa pesa hizo.
Comments